Genesis 24:1-6

Isaka Na Rebeka

1 aWakati huu Ibrahimu alikuwa mzee mwenye miaka mingi, naye Bwana alikuwa amembariki katika kila njia. 2 bAkamwambia mtumishi wake mkuu wa vitu vyote katika nyumba yake, yule aliyekuwa msimamizi wa vitu vyote alivyokuwa navyo, “Weka mkono wako chini ya paja langu, 3 cNinataka uape kwa Bwana, Mungu wa mbingu na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke kutoka binti za Wakanaani, ambao ninaishi miongoni mwao, 4 dbali utakwenda katika nchi yangu na jamaa zangu umpatie Isaka mwanangu mke.”

5 eYule mtumishi akamuuliza, “Je, kama huyo mwanamke atakataa kuja nami katika nchi hii? Je, nimpeleke mwanao katika hiyo nchi uliyotoka?”

6Ibrahimu akasema, “Hakikisha kwamba hutamrudisha mwanangu huko.
Copyright information for SwhKC